Pandeolwa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Pandeolwa (pia wanda; kwa Kiing. dimension) ni dhana katika hisabati na fizikia inayoeleza tabia za kiolwa katika nafasi kilichomo. Kwa maarifa yetu ya kawaida tunatofautisha pandeolwa tatu ambazo ni upana, urefu na kina / kimo.

Kwa maana hiyo mstari una pandeolwa mmoja, eneo kama mraba au mviringo huwa na pandeolwa mbili, gimba kama mchemraba au tufe huwa na pandeolwa tatu.
Ulimwengu mara nyingi huelezwa kuwa na pandeolwa nne, yaani urefu, upana, kimo na wakati.
Katika hisabati kuna nafasi ya kuangalia pandeolwa nyingine na zaidi.
Tofauti ya pandeolwa hutajwa mara nyingi kwa kifupi cha Kiingereza kama "2-d" au "3-d" yaani "2 dimensions" au "3 dimensions".
Remove ads
Istilahi
Hadi sasa hakuna mapatano kamili kuhusu istilahi inayoweza kutaja "dimension" ya Kiingereza. KAST ilitumia "wanda, mawanda"[1]. Masomo yanayoandaliwa na mtandao wa TESSA[2] hutumia "pandeolwa".
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads