Soko la Hisa la Nairobi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Soko la Hisa la Nairobi (NSE) ndilo soko kuu la kuuza na kununua Hisa nchini Kenya. Lilianza mwaka wa 1954 kama Soko la Hisa la Ng'ambo wakati Kenya ilikuwa bado chini ya Ukoloni wa Uingereza kwa ruhusa ya Soko la Hisa la London. NSE ni mwanachama wa Shirikisho la Masoko ya Hisa ya Afrika.
Taswira
Soko la Hisa la Nairobi ndilo la nne kwa ukubwa Afrika katika mtazamo wa idadi ya hisa zinazouzwa, na la tano katika Thamani ya Hisa zote kama asilimia ya Pato la Taifa.[1] Soko hili hufanya kazi kwa ushirikiano na Soko la Hisa la Uganda na Soko la Hisa la Dar-es-Salaam, pamoja na kusajili hisa mbalimbali katika masoko yote matatu.
Soko hili lina vikao vya kabla kati ya 09:00-09:30 na vikao vya biashara ya kawaida kati ya 09:30-03:00 siku zote za wiki isipokuwa Jumamosi, Jumapili na sikukuu zinazotangazwa na Soko mapema.[2]
Ofisi na sakafu ya biashara za NSE ziko katika jumba la Nation Centre katika baraste ya Kimathi. Biashara hufanywa kupitia Electronic Trading System (ETS) ambayo ilikamilika mwaka wa 2006. Mtandao wa Wide Area Network (WAN) uliwekwa mwaka wa 2007 na hili lilitupilia mbali haja ya Kampuni za kuuza na kununulia Hisa kuwapeleka mawakala wao (wafanyabiashara) kwenye ukumbi wa biashara ili kuuza au kununua hisa. Kwa sasa, shughuli za kununua na kuuza hufanywa kutoka ofisi zao kupitia mtandao wa WAN. Hata hivyo, baadhi ya mawakala bado wanaweza kufanya biashara kutoka sakafu ya NSE.
Fahirisi mbili hutumiwa kwa kawaida kupima utendaji. Ile ya NSE 20-Share Index imetumiwa tangu mwaka wa 1964 na hupima utendaji wa kampuni 20 bora zilizo na msimamo mzuri kifedha na ambazo zimezidi kurejesha matokeo mazuri ya kifedha mfululizo. Zilizojumuishwa katika fahirisi hii ni Kampuni ya Sukari ya Mumias, Express Kenya, Rea Vipingo, Sasini Tea, CMC Holdings, Kenya Airways, Safaricom, Nation Media Group, Barclays Bank Kenya, Equity Bank, Kenya Commercial Bank, Standard Chartered Bank, Bamburi Cement, British American Tobacco, Kengen, Centum Investment Company, East African Breweries, EA Cables, Kenya Power & Lighting Company Ltd na Athi River Mining. Fahirisi hii haswa hulenga mabadiliko ya bei ya makampuni haya 20.
Mwaka wa 2008, NSE All Share Index (NASI) ilianzishwa kama fahirisi mbadala. Kipimo chake ni kiashiria cha utendaji wa soko kwa jumla. Fahirisi hii hujumuisha hisa zote zilizouzwa au kununuliwa kila siku. Hivyo basi mtazamo wake ni utendaji kwa ujumla wa thamani ya hisa zote katika soko badala ya mabadiliko ya bei ya Hisa chache teule.
Hata hivyo kuna fahirisi nyingine ya tatu; AIG 27 Index ambayo hulinganishwa mabadiliko ya bei ya hisa za makampuni 27 ambazo zimetambuliwa kama zilizo imara kiasi. Wazo la msingi la fahirisi hii inalingana na ile ya NSE 20-Share Index. Lakini ilhali ile ya AIG imebainishwa na kampuni ya AIG (kampuni ya huduma za kifedha na sehemu ya AIG Group), ile ya NSE 20-share Index ni ya Soko la Hisa la Nairobi.
Remove ads
Kampuni zilizosajilishwa
Kampuni zilizokuwa zimesajilishwa kufikia Agosti 2015:
Sekta ya kilimo
Magari na Vifaa
Fedha
Huduma za kibiashara
Ujenzi na Muhimbili
Kawi na Mafuta
Bima
Uwekezaji
Huduma za uwekezaji
Viwanda na Muhimbili
Mawasiliano na Teknolojia
Sehemu ya kampuni ndogo
Soko la Mapato yasiyobadilika
(FISMS)
Remove ads
Viungo vya nje
- Tovuti ya Soko la Hisa La Nairobi
- Capital Markets Authority, Kenya - shirikisho la kitaifa la kusimamia masoko ya mitaji nchini Kenya, ikiwa ni pamoja na Soko la Hisa la Nairobi Ilihifadhiwa 28 Juni 2023 kwenye Wayback Machine.
- KenInvest - shirikisho la kitaifa la uwekezaji na biashara
- Soko la Hisa la Nairobi kutoka tovuti ya Adam Rosen.
- Historia na maelezo kuhusu Soko la Hisa la Nairobi kutoka MBendi Ilihifadhiwa 21 Mei 2023 kwenye Wayback Machine.
- Shirikisho la Masoko ya Hisa ya Africa Ilihifadhiwa 23 Februari 2007 kwenye Wayback Machine.
Tazama Pia
- Uchumi wa Kenya
- Orodha ya masoko ya hisa barani Afrika
- Orodha ya masoko ya hisa
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads