Najida
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Najida (ing. na lat. Bellatrix pia γ Gamma Orionis, kifupi Gamma Ori, γ Ori) ni nyota angavu ya tatu katika kundinyota la Jabari (Orion). Na pia ni nyota angavu ya 25 kwenye anga ya usiku.
Remove ads
Jina
Najida ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [1]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wakitafsiri jina lao النجيد al-najid linalomaanisha „shujaa, mtu hodari au pia simba" [2] ; jina la Waarabu lilitafsiriwa na wataalamu wa Ulaya kwa jina la Kilatini Bellatrix (“askari au mpiganaji wa kike”) [3]
Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kilatini na kuorodhesha nyota hii kwa jina la "Bellatrix" [4] .
"Gamma Piscis" ni jina la Bayer maana ina nafasi ya tatu kufuatana na mwangaza katika kundinyota lake.
Remove ads
Tabia
Najida - Bellatrix ni nyota maradufu yenye pacha 2-3 zinazotajwa kama α Orionis Austrini A, B na C. Iko mbali na Dunia kwa miakanuru 25. α Orionis Austrini A ni Bellatrix yenyewe, iko kwenye safu kuu yenye mwangaza unaoonekana wa Vmag 1.17. Masi ya Najida (nyota A) ni M☉ 1.92 na nusukipenyo chake R☉ 1.84 (vizio vya kulinganisha na Jua letu) . Mwangaza halisi ni 1.1 ikiwa katika kundi la spektra A3 V.[5].
Ikiwa ni nyota jitu yenye rangi ya buluu katika kundi la spektra B2 masi yake ni mara nane ya Jua na mng'aro ni mara 9000 wa Jua. Baada ya miaka milioni kadhaa itapanuka na kuwa jitu jekundu. Masi yake haitoshi kuishia katika mlipuko kwa hiyo itaishia kama nyota kibete cheupe chenye masi kubwa.
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya Nje
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads