Shahada (Uislamu)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Shahada (Uislamu)
Remove ads

Shahada ni ungamo wa imani ya Kiislamu.

Ukweli wa haraka
Thumb
Shahada kama mapambo kwenye ukuta wa msikiti wa Wazir Khan mjini Lahore (Pakistan)
Thumb
Shahada kwenye bendera ya Uarabuni wa Saudia

Tamko hili lina maneno yafuatayo: لا إله إلا الله محمد رسول الله (Lā ilāhā illā-llāhu; muhammadun rasūlu-llāhi). Maana yake ni: "Hakuna mungu ila Allah; Muhammad ni mtume wa Allah". Katika sala maneno haya huanzishwa kwa "أشهد أن‎" (ash-hadu an yaani: Nakiri kwamba...).

Kwa maneno haya Mwislamu hutamka kuwa

  • Mungu (Allah) ni mmoja tu hakuna mwingine
  • Muhammad ni mtume na rasul wake wa mwisho.

Shahada ni moja ya nguzo tano za Uislamu. Hurudiwa kila siku na Mwislamu akifuata wajibu wake wa sala.

Kuna Washia kadhaa wanaoongeza maneno "Alīyun wali Allah" (علي ولي الله - "Ali rafiki yake Mungu") wakitaka kukiri ya kwamba katika imani yao Ali ni kiongozi teule wa Waislamu.

Kutamka shahada kwa imani ni tendo la kujiunga na Uislamu na kuwa Mwislamu.

Remove ads

Historia

Mfano wa kale wa shahada uko kwenye maandiko yaliyopo kwenye ukuta wa nje wa msikiti wa Kubba ya Mwamba mjini Yerusalemu uliojengwa kwa amri ya khalifa Abd al-Malik ibn Marwan mnamo mwaka 691. Hapa ina umbo lifuatalo: لا اله إلا الله وحده لا شريك له محمد رسول الله ‎ / la ilaha ila allahu wahdahu la sharika la-hu Muhammadun rasulu ʾllah(i) /„Hakuna mungu ila Allah peke, hana mwenzake, Muhammad ni mtume wa Allah". Sehemu yenye maneno yasiyotazamiwa leo kuwa sehemu ya shahada "lā šarīka la-hu" ni kutoka Kurani sura 6, 163.

Umbo jinsi nilivyo leo ni mapatano kati ya madhehebu ya Kisunni.

Thumb
Bendera ya Somaliland inaonyesha shahada
Remove ads

Matumizi ya kisiasa

Kuna bendera ya nchi kadhaa zinazoonyesha shahada:

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads