Neli (ndege)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Neli (ndege)
Remove ads

Neli ni ndege wadogo wa jenasi kadhaa katika familia Nectariniidae. Spishi hizi ni kama chozi lakini kubwa kuliko spishi nyingi za chozi. Takriban spishi zote zina rangi ya majani. Manyoya ya kati ya mkia ni marefu sana katika spishi za Nectarinia. Domo lao limepindika na hutumika kwa kutoa mbochi katika maua au wadudu katika matundu. Hula mbochi hasa na pengine maji ya matunda na wadudu pia. Ndege hawa wanatokea Afrika kusini mwa Sahara. Tundu lao lina umbo la mfuko na limening'izika kwa vitawi vyembamba. Jike hutaga mayai 2-4.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Spishi za Afrika

Remove ads

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads