Ngano nyekundu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ngano nyekundu
Remove ads

Ngano nyekundu (lat. Secale cereale; ing. rye) ni mmea wa familia ya manyasi katika ngeli ya monokotiledoni. Mbegu au punje za ngano nyekundu ni nafaka ambayo ni chakula muhimu katika sehemu za dunia hasa kwenye kanda zisizo na joto au baridi kali. Ni mmea ulio karibu na ngano.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...
Thumb
Secale cereale

Matumizi yake ni kwa ajili ya unga, mkate, bia, aina za wiski na pombe mbalimbali halafu lishe ya wanyama.

Ngano nyekundu hustawi kwenye ardhi ya mchanga ambako ngano haiendelei vizuri inavumilia pia tofauti kubwa zaidi za mvua na ukame kuliko ngano.

Remove ads

Kilimo chake na matumizi

Maelezo zaidi Nchi walima wakuu wa ngano nyekundu — 2005 (millioni t³) ...


Ngano nyekundu hulimwa hasa katika nchi za Ulaya ya Mashariki, ya kati na kaskazini kama vile Ujerumani, Polandi, Ukraine, Belarusi, Lithuania, Latvia hadi Urusi. Hulimwa pia katika Amerika ya Kaskazini (Kanada na Marekani), katika Amerika Kusini (Argentina), Uturuki, Kazakhstan na China ya kaskazini.

Katika Afrika imelimwa kidogo kwenye nyanda za juu za Tanzania pia Kenya.

Remove ads

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads