Ukraini
nchi katika Ulaya ya Mashariki From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ukraini, rasmi kama Jamhuri ya Ukraini, ni nchi katika Ulaya ya Mashariki, inapakana na Belarus kaskazini, Russia mashariki, Bahari Nyeusi kusini, Moldova na Romania kusini magharibi, na Hungary, Slovakia, na Polandi magharibi. Ina idadi ya watu takriban milioni 36, ikiwa ya 41 duniani. Jiji lake kubwa zaidi ni Kyiv, ambalo pia ni mji mkuu.

Remove ads
Historia
Historia ya kale

Vyanzo vya Ukraini ni pamoja na vile vya Urusi wakati ambako [[|kabila|makabila]] ya wasemaji wa Kislavoni cha Mashariki walikoanza kujenga maeneo yao kuanzia karne ya 8 BK.
Waviking kutoka Skandinavia waliunda miji ya biashara na dola la kwanza katika eneo la Kiev. Wenyewe waliingia haraka katika lugha na utamaduni wa Waslavoni wenyeji, lakini waliacha jina lao "Rus" ambalo kiasili lilikuwa jina la Waskandinavia wale kutoka Uswidi ya leo.
Mwaka 988 mtawala wa Kiev alipokea Ukristo wa Kiorthodoksi kutoka Bizanti. Aliagiza wananchi wabatizwe pamoja naye ambayo inakumbukwa kama "Ubatizo wa Urusi". Tukio hilo liliathiri moja kwa moja utamaduni na historia yote iliyofuata.
Dola la Kiev liliporomoka kutokana na mashambulio ya Wamongolia baada ya Jingis Khan waliovamia na kuchoma Kiev mnamo mwaka 1240. Milki iligawiwa na temi ndogo zilijitokeza zalizopaswa kukubali ubwana wa Wamongolia.
Baina ya Polandi, Lituanya na Utemi wa Moscow
Katika karne ya 14 sehemu kubwa ya maeneo ya Milki ya Kiev ya awali ilifikishwa chini ya utawala wa Polandi na Lituanya. Tawi moja la familia ya watawala wa Kiev lilidhibiti Moscow katika mashariki-kaskazini. Hapa viongozi wake walifaulu kuimarisha utawala na kupanusha eneo lake. Hata askiofu mkuu wa Kiev aliyepaswa kuondoka baada ya kuchomwa wa mji wake hatimaye alihamia Moscow. Hivyo watawala wa utemi wa Moscow walijitazama kama wafuasi halali wa Dola la Kiev wakaendelea kutumia jina "Rus" lililoendelea kuwa chumbukizo la jina Urusi. Hatimaye watemi wa Moscow walifaulu kushinda pia Wamongolia na kupata uhuru.

Maeneo makubwa ya Ukraini ya leo yalikuwa chini ya utawala wa Lituanya na Polandi na baadaye ya Ufalme wa Maungano ya Polandi-Lituanya. Mwaka 1696 watawala wa Polandi walishawishi sehemu ya maaskofu Waorthodoksi kukubali maungano na kanisa katoliki na hii ilikuwa chanzo cha kutokea kwa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraini.
Sehemu ya Ukraini upande wa mashariki wa mto Dnestr ilitawaliwa na Moscow.
Katika karne ya 18 Polandi iligawanywa kati ya majirani yake. Ugawaji huo uliongeza sehemu za Ukraini zilizofika chini ya utawala wa Urusi. Ila sehemu ya kusini-magharibi ilikuwa sehemu ya milki ya Austria. Katika maeneo chini ya Urusi Wakatoliki walipaswa kurudi katika Kanisa la Kiorthodoksi. Lakini katika maeneo yaliyochukuliwa na Austria tangu mwaka 1772, serikali iliwapa Wakatoliki Waukraini haki sawa na Kanisa la Kilatini; liliweza kuunda seminari na vyuo; taasisi hizo zikawa chimbuko la kukua kwa lugha ya Kiukraini na utaifa wa Kiukraini.

Mnamo 1775, ngome ya mwisho ya Cossacks ya Kiukreni, ngome ya Sich, iliharibiwa na askari wa kifalme wa Kirusi waliokuwa wakitoka Ngome ya Mtakatifu Elizabeth, wakati huo kituo kikuu cha kijeshi cha Dola ya Kirusi huko Ukraine. Uharibifu wa Cossacks ulisababisha utumwa wa Waukraine na sera ya Urusishaji (kwa Kirusi: Русификация) - kupiga marufuku rasmi na uharibifu wa lugha na utamaduni wa Kiukreni na wakoloni wa Kirusi. Mfano wa kushangaza zaidi wa sera kama hiyo ni Amri ya Ems (kwa Kirusi: Эмский указ) na amri ya Piotr Valuev (kwa Kirusi: Валуевский циркуляр) Waziri wa Mambo ya Ndani ya Dola ya Urusi, hati hii kutoka 1863 ilisema kwamba lugha ya Kiukreni "haikuwepo, haipo na haiwezi kuwepo, na mtu yeyote ambaye hakubaliani na taarifa hii ni adui wa Urusi." [1][2][3].
Karne ya 20

Mnamo 1914, Mtawala Nikola II wa Urusi alipiga marufuku sherehe ya kumbukumbu ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa mwandishi mkuu wa Kiukreni Taras Shevchenko, ambayo iliambatana na kukamatwa kwa watu wengi na kufungwa gerezani[4].
Mapinduzi ya Februari ya 1917, yaliyoongozwa na Alexander Kerensky, yalipindua utawala wa kifalme na kuunda jamhuri ya Kirusi, na kuwapa watu wengi waliokuwa watumwa na Warusi fursa ya kupigania uhuru wao. Kerensky mwenyewe alisema, "Ikiwa Dola ya Urusi imepita manufaa yake, anguko lake lazima lianzie Kyiv".
Lakini mwishoni mwa 1917, Vladimir Lenin, ambaye aliingia madarakani na kutangaza vita vya wenyewe kwa wenyewe, aliunda serikali bandia ya Kisovieti ya Kiukreni huko Kharkiv (megalopolis mashariki mwa nchi) na kutangaza vita dhidi ya Ukraine, ambayo iliambatana na Ugaidi Mwekundu na uhalifu mkubwa, kama vile kufyatua risasi kwa Kyiv kwa kutumia silaha za kemikali mnamo Februari 4, 1918, na Ugaidi Mwekundu - mauaji makubwa ya raia, mnamo Machi 1918, askari wa harakati ya uhuru wa Kiukreni waligundua kwamba mbuga za Kyiv, baada ya kurudi nyuma kwa wanajeshi wa Soviet, zilijazwa na mamia ya maiti zilizoharibika za raia ambao walikufa kutokana na kuteswa na huduma ya siri ya Usovieti, Cheka.

Miaka 1918 - 1921 baada ya mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na ya kuporomoka kwa Milki ya Urusi nchi ilikuwa na kipindi kifupi cha uhuru na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Baada ya ushindi wa wakomunisti, nchi iliungwa katika Umoja wa Kisovyeti kama kuwa Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiukraini kati ya 1922 - 1991 .
Baada ya mwaka 1927 Wakomunisti chini ya Stalin waliamua kufuta mali binafsi ya ardhi wakalazimisha wakulima wote kulima kw muundo wa ujamaa. Sisa hii ilisababisha njaa mbaya sana katika Ukraini kwenye miaka 1930-1932 ambamo Waukraini milioni 4 hivi walikufa njaa.
Mnamo 1937, NKVD (baadaye iliitwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Umoja wa Kisovieti) iliteka nyara kwa siri na kuwatesa/kuwapiga risasi zaidi ya wawakilishi mia moja wa wasomi wa Kiukreni na takwimu za elimu na sinema ambao walikuwa wakipigania uhuru wa Ukraine. Miili yao ilizikwa kwa siri katika msitu wa Bykivnya karibu na Kyiv, ambapo kumbukumbu iliundwa baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti[5].

Vita Kuu ya Pili ya Dunia kwenye Umoja wa Kisovyeti ilipiganiwa sana katika Jamhuri ya Kisovyeti ya Ukraini. Wajerumani waliua raia wa Kiyahudi milioni na nusu, kwa jumla walikufa Waukraini milioni 5-6 wakati wa vita. Mnamo 1941-1945 Wanazi waliua raia mmoja kati ya watano wa Ukrain wakati wa kuikalia nchi hiyo.
Mwishoni mwa Muungano wa Sovieti, viongozi waliwafunga wapinzani, maarufu zaidi kati yao alikuwa Vasyl Stus. Saikolojia ya kuadhibu pia ilikuwa maarufu sana dhidi ya wapinzani wa kisiasa na kiitikadi, mada za Njaa ya 1932-1933 na ukandamizaji mkubwa wa kisiasa zilikuwa mwiko kwa majadiliano. Na mnamo 1985-1991 tu ndipo Umoja wa Kisovieti ulipoanguka kama matokeo ya mageuzi ya kidemokrasia.
Uhuru tangu 1991
Wakati wa kuporomoka wa ukomunisti Umoja wa Kisovyeti ilifutwa, hivyo Ukraini ilipata uhuru wake. Ndani ya nchi na siasa yake yalitokea mawazo tofauti kuhusu mwelekeo; walioshindana walikuwa hasa wale waliotaka kuelekea uanachama na Umoja wa Ulaya na wengine waliotafuta ushirikiano wa karibu zaidi na Urusi.
Mwaka 1991 Urusi na Ukraini ziliutia sahihi mkataba wa urafiki walipoahidiana kuheshimiana kama majirani wema.
Kwa msingi huo, mwaka 1994 Ukraini ilikabidhi Urusi silaha za nyuklia iliyowahi kurithi kutoka jeshi la Kisovyeti na kwenye Mkataba wa Budapest Urusi, Marekani na Uingereza ziliahidi kulinda Ukraini katika mipaka yake dhidi ya mashambulizi yoyote[6].
Hata hivyo, baada ya mwaka 2000 majadiliano ndani ya Ukraini kuhusu kujiunga na umoja wa NATO ilianza kuleta ugumu katika uhusiano na Urusi.
Mwaka 2013 yalitokea maandamano na mapigano kwa sababu rais Viktor Yanukovich aliamua ghafla kukataa mapatano ya kujiunga na Umoja wa Ulaya yaliyokwisha kukubaliwa tayari. Waandamanaji kwa mamia waliuawa na polisi na hatimaye rais alikimbilia Urusi. Hapo bunge liliamua kumwondoa madarakani na kuwa na uchaguzi mpya wa rais.

Katika hali hiyo Urusi ilivamia Krim kwa njia ya kuficha. Wanajeshi wasio na sare walitokea kwenye miji ya Krim wakivamia majengo ya serikali pamoja na bunge la kieneo[7]. Idadi isiyojulikana ya wabunge la jimbo la Krim waliamua tarehe 5 Februari kuondoa serikali ya jimbo wakaitisha kura za wananchi. Tarehe 11 Februari walitangaza uhuru wa Krim, na kura ya wananchi ya tarehe iliyoendeshwa na mamlaka mpya ilitangaza kuwa na kura nyingi za kujiunga na Urusi. Ombi hilo lilikubaliwa na Urusi.
Mnamo Aprili 2014 waandamanaji walivamia majengo ya serikali huko Donetsk wakidai pia kura kuhusu kujitenga na Ukraini. Baada ya kuondolewa na polisi, waandamanaji wenye silaha walitangaza maeneo ya Donetsk na Luhansk kuwa "jamhuri za kujitegemea". Serikali ya Ukraini iliongeza polisi na pia jeshi. Mapigano yalianza ambako jeshi la Urusi lilisaidia waasi, kwanza kwa siri na baadaye waziwazi. Mapigano hayo yalikuwa mwanzo wa Vita ya Donbas iliyoendelea hadi mwaka 2022[8] [9][10][11].

Mwaka 2022 rais wa Urusi alitangaza kwamba yeye haoni Ukraini kama nchi halisi akaamuru jeshi lake kuvamia Ukraini tarehe 24 Februari[12]. Urusi inatenda uhalifu mkubwa wa kivita kama vile kulipua maeneo ya makazi, kuharibu miji mizima kama Mariupol, kuunda "kambi za uchujaji", kutesa raia, kubaka wanawake, kuua wazazi mbele ya watoto wao na kuwahamisha raia wa Ukraine kwa nguvu kwenda Urusi, kuwanyima wagonjwa dawa na kuwatesa raia wao wenyewe, Warusi, kwa msimamo wao wa kupinga vita. Kitendo cha aibu zaidi cha jeshi la Urusi kilikuwa mauaji katika mji wa Bucha, mkoa wa Kiev [13] [14] [15].[16] [17].
Remove ads
Wakazi
Sensa ya mwaka 2001 ilionyesha ya kwamba 77.8% za wakazi hujiita "Waukraini". Waliojiita Warusi walikuwa 17.3%. Vikundi vingi vingine kama Wabelarusi, Wamoldova, Watartari, Wabulgaria, Wapolandi, Wayahudi na wengine walikuwa kila kimoja chini ya 1%.
Lugha
Kwa muda mrefu Ukraini ilitawaliwa na Urusi na Kirusi kilikuwa lugha ya utawala hali halisi. Hivyo wengi wamezoea Kirusi, hata kati ya Waukraini asilia; hivyo Kiukraini kilikuwa lugha mama ya 67.5%, Kirusi ya 29.6%.
Tangu uhuru serikali imeendesha sera ya kujenga lugha ya taifa, pamoja na kujali lugha nyingine 18 za kieneo.
Hivyo lugha rasmi ni Kiukraini (українська мова "ukrajin's'ka mova"), mojawapo kati ya lugha za Kislavoni, karibu sana na Kirusi, lakini angalau nusu ya wakazi hutumia pia Kirusi.
Dini
Baada ya ukomunisti kupiga vita dini kwa njia zote na kwa miaka mingi, siku hizi wakazi wengi wamerudia dini zao.
Walionayo ni hasa Wakristo (81.9%), wakiwemo wale wa Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi (23%), lakini Waorthodoksi wengine wamejitenga na kuanzisha Kanisa la Kiorthodoksi la Ukraini (40.8%).
Pia kuwa waamini wengiwengi wa Kanisa Katoliki (10.2%), hasa wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraini (9.4%) linalofuata mapokeo ya Kigiriki kama Waorthodoksi, lakini pia wa Kanisa la Kilatini (0.8%).
Waprotestanti ni 2.2% na Waislamu 1.1%.
Pamoja na hayo, idadi ya wakazi inazidi kupungua haraka (-12.8% kati ya 1993 na 2014).
Remove ads
Tazama pia
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads