Ngono zembe

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ngono zembe
Remove ads

Ngono zembe maana yake ni tendo la ndoa lililofanywa au linalofanywa kwa uzembe, yaani bila kujali matokeo yake, hasa maambukizi ya maradhi ya zinaa, na kwa namna ya pekee Ukimwi.

Thumb
Tangazo la Marekani dhidi ya uzinifu wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Katika jamii, na hata mbele ya Mungu ni kosa kusababisha madhara bila sababu, hasa kama ni kuendeleza maradhi yanayomtesa binadamu, yanahitaji tiba ya gharama kubwa, na hatimaye yanaweza kuleta kifo cha wengi.

Baadhi ya watumiaji wanataka kumaanisha kufanya ngono bila kondomu, kama kwamba kutumia mpira huo kungetosha kuleta usalama kwa wahusika. Kumbe siyo, kwa sababu kondomu inapunguza uwezekano wa maambukizi (katika nchi zilizoendelea kwa asilimia 70-85), lakini haiwezi kuyazuia kabisa[1][2].

Kinyume chake, inawezekana kufanya tendo la ndoa bila kondomu wala uzembe kwa sababu linafanywa na watu waaminifu wasio na ugonjwa wa namna hiyo. Hivyo wako salama tu.

Tafiti kadhaa bara Afrika zimeonyesha kwamba tohara inaweza kupunguza maambukizi ya wanaume kwa asilimia 60[3], lakini wengine wanapinga.[4][5]

Kwa vyovyote Kusini kwa Sahara mabadiliko ya tabia na matumizi ya kondomu yameonekana kufanikiwa zaidi na bila gharama ya tohara.[6]

Remove ads

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads