Nouakchott

From Wikipedia, the free encyclopedia

Nouakchott
Remove ads

Nouakchott (Kiarabu: نواكشوط) ni mji mkuu wa Mauritania. Uko mwambaoni mwa Atlantiki magharibi mwa nchi. Idadi ya wakazi imekadiriwa kupita milioni moja.

Ukweli wa haraka Nchi ...
Thumb
Mahali pa Nouakchott nchini Mauretania.
Thumb
Matuta ya mchanga kando ya Nouakchott.

Historia

Hadi 1958 Nouakchott ilikuwa kijiji kidogo cha wavuvi. Imekua tangu uhuru. Wakati wa ukoloni Mauritania haikuhesabiwa kama eneo la pekee: ilikuwa sehemu tu ya Afrika ya Magharibi ya Kifaransa yenye mji mkuu wa Saint-Louis huko Senegal.

Baada ya azimio la kugawa eneo la Kifaransa katika Afrika ya Magharibi Nouakchott ikateuliwa kuwa mji mkuu ujao na mradi wa ujenzi ulilenga kuongeza idadi ya wakazi hadi kufikia watu 15,000. Baada ya uhuru mwaka 1962 mji ukawa mji mkuu wa Mauritania.

Katika miaka ya 1970 idadi ya wakazi iliongezeka sana kutokana na ukame uliofukuza watu wengi mashambani, kati ya miaka 1969 na 1980 kutoka wakazi 20,000 kufikia 150,000.

Siku hizi mju una tatizo zito la uhaba wa maji kwa wakazi wake wengi.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads