Mauritania
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mauritania ni nchi ya Afrika kaskazini-magharibi. Upande wa magharibi kuna pwani ya bahari ya Atlantiki, upande wa kusini imepakana na Senegal, upande wa mashariki na Mali na Algeria, upande wa kaskazini na Sahara ya Magharibi inayotawaliwa na Moroko. Mji mkuu ni Nouakchott. Mji wa pili na kitovu cha uchumi ni bandari ya Nouadhibou karibu na mpaka wa Sahara Magharibi.
Jina limeteuliwa kutokana na Mauritania ya kale iliyokuwa ufalme wa Waberber kusini kwa Mediteranea katika eneo la Algeria na Moroko ya leo.
Remove ads
Wilaya za Mauritania
Mauritania ina wilaya 12 (zinaitwa "wilāyah").
![]() |
Siasa ya Mauritania
Mnamo Machi 2007 wananchi walipata nafasi ya kumchagua rais kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi tangu uhuru. Sidi Ould Cheikh Abdallahi alishinda katika duru ya pili kwa 53% za kura zote akaapishwa tarehe 20 Aprili 2007. Lakini mwaka 2008 JeneralI Mohamed Ould Abdel Aziz alimpindua, akashinda uchaguzi miaka 2009 na 2014. Baada ya uchaguzi wa mwaka 2019 alianza kutawale jenerali Mohamed Ould Ghazouani na serikali yake isiyojali sana haki za binadamu.
Remove ads
Watu
Wakazi wengi (70%) ni Wamori, mchanganyiko wa Waarabu, Waberber na Waafrika waliotokana na watumwa kutoka kusini kwa Sahara. Asilimia 30 zilizobaki ni makabila ya Kiafrika yasiyoongea Kiarabu, ambacho ndicho lugha rasmi.
Pamoja na hayo, hadi leo asilimia 2.1 za wakazi ni watumwa, ingawa mwaka 2007 ilifutwa haki ya kuwamiliki.
Upande wa dini, karibu wote ni Waislamu (hasa Wasuni). Uhuru wa dini unabanwa sana kwa nyingine zote na ukanamungu unaadhibiwa kwa kifo. Wakristo ni 10,000 hivi, karibu wote wageni.
Tazama pia
Marejeo
- Foster, Noel (2010). Mauritania: The Struggle for Democracy. Lynne Rienner Publishers. ISBN 978-1935049302.
- Hudson, Peter (1991). Travels in Mauritania. Flamingo. ISBN 978-0006543589.
- Murphy, Joseph E (1998). Mauritania in Photographs. Crossgar Press. ISBN 978-1892277046.
- "Slavery's last stronghold". CNN. Iliwekwa mnamo 3 Februari 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Pazzanita, Anthony G (2008). Historical Dictionary of Mauritania. Scarecrow Press. ISBN 978-0810855960.
- Ruf, Urs (2001). Ending Slavery: Hierarchy, Dependency and Gender in Central Mauritania. Transcript Verlag. ISBN 978-3933127495.
- Sene, Sidi (2011). The Ignored Cries of Pain and Injustice from Mauritania. Trafford Publishing. ISBN 978-1426971617.
Remove ads
Viungo vya nje
- (Kifaransa) (Kiarabu) (Kiingereza) Serikali ya Mauritania
- Mauritania entry at The World Factbook
- Mauritania katika Open Directory Project
- Mauritania profile from the BBC News.
- Wikimedia Atlas of Mauritania
- Forecasts for Mauritania Development
- US State Department
- Encyclopædia Britannica, Mauritania – Country Page
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mauritania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads