Kanga (ndege)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kanga (ndege)
Remove ads

Kanga ni ndege wa familia Numididae. Jina hili ni jina la kawaida la ndege hawa, lakini spishi za Afrika ya Mashariki wana majina mengine kama chelele, chepeo, kololo, kororo na kicheleko (tazama orodha ya spishi). Kanga ni wakubwa kuliko kwale na wana rangi nyeusi na madoa meupe. Kichwa chao hakina manyoya lakini spishi tatu zina manyoya juu ya utosi. Kanga mweusi na kanga kidari-cheupe hawajulikani sana, lakini mwenendo wao unasadikiwa kufanana na ule wa spishi nyingine. Hula mbegu, wadudu, makoa na nyungunyungu, na hutaga mayai ardhini. Kanga huwa mwenzi mmoja tu maisha yao yote.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...

Spishi zote zinatokea Afrika. Chepeo hufugwa hususa huko Afrika ya Magharibi na pia katika Ulaya na Marekani.

Remove ads

Spishi

Picha

Viungo vya Nje

Ukweli wa haraka
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads