Nyigu-kekeo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Nyigu-kekeo (kutoka kwa Kiing. cuckoo wasps) ni nyigu waliotaga mayai yao katika viota vya nyigu wengine kama kekeo wanavyofanyia ndege wengine. Kuna makundi mbalimbali ya nyigu-kekeo. Familia iliyoenea zaidi na kuwa na spishi nyingi barani Afrika ni Chrysididae yenye spishi 55 katika Afrika ya Mashariki. Jenasi Ceropales ya familia Pompilidae ina spishi 10 za nyigu-kekeo katika Afrika ya Mashariki na kuna spishi 3 katika nusufamilia Bembicinae ya familia Crabronidae. Spishi nyingine za nyigu-kekeo hazitokei Afrika.
Remove ads
Maelezo
Kwa sababu nyigu hawa wako katika makundi mbalimbali ya kitaksonomia, haiwezekani kutoa maelezo ya wao wote pamoja. Tembelea kurasa maalum kwa habari zaidi. Hata hivyo, kwa ujumla, nyigu hawa huwa na kutikulo ngumu kuhimili mashambulizi ya mbuawa wao. Kwa sababu hiyo hiyo, wanaweza kuwa na marekebisho mengine. K.m. spishi za Chrysididae zinaweza kujiviringa katika tufe ili kulinda miguu yao na sehemu za chini za kichwa.
Kama jina lao linavyoonyesha, nyigu hawa wana tabia kama kekeo kwa maana kwamba wao pia hawajengi viota vyao wenyewe, lakini hutaga mayai kwenye viota vya nyigu wengine, kwa kawaida wapweke. Mara nyingi wanadusia spishi moja ya mdusiwa tu au spishi chache.
Remove ads
Spishi za Afrika ya Mashariki
Crabronidae
Chrysididae
|
Pompilidae
|
Remove ads
Picha
- Stizoides renicinctus
- Stilbum cyanurum
- Trichrysis cyanea
- Ceropales maculata
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads