Onesiforo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Onesiforo (jina la Kigiriki lenye maana ya "mleta faida") alikuwa mwanamume Mkristo wa karne ya 1 aliyetajwa na Mtume Paulo kwa shukrani katika Waraka wa pili kwa Timotheo 1:16-18.

Sababu ni kwamba alimsaidia sana alipokuwa Efeso, halafu akamfuata hadi Roma mpaka akafaulu kumuona na kumfariji bila kuonea aibu minyororo yake.[1][2][3]
Kwa hiyo Paulo alimtakia huruma ya Mungu pamoja na familia yake.[4]
Inasemekana Onesiforo alipata kuwa askofu wa Kolofon (Asia Ndogo), halafu wa Korintho. Hatimaye alifia dini mjini Parium (karibu na Efeso)[5].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Septemba[6][7] au kesho yake[8].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads