Onesimo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Onesimo
Remove ads

Onesimo (kwa Kigiriki Ὀνήσιμος, Onēsimos, yaani "Wa kufaa"; labda alifia dini Roma, Italia, mwaka 68 hivi),[1] alikuwa mtumwa wa Filemoni, Mkristo tajiri wa Kolosai, leo nchini Uturuki.

Thumb
Picha ya kifodini cha Onesimo, kutoka Menologion ya Basili II (1000 BK hivi).

Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15[2] au 16 au 28 Februari, au tarehe 22 Novemba.

Remove ads

Katika Biblia

Jina "Onesimo" linatajwa katika Nyaraka mbili za Mtume Paulo: Waraka kwa Wakolosai 4:9[3] na Waraka kwa Filemoni ambao uliandikwa wote ili kumtetea.

Ni kwamba Onesimo alikuwa amemkimbia Filemoni na labda alimuibia pia. Lakini baadaye alikutana na Mtume Paulo (ama Roma ama Kaisarea)[4][5] akaongokea Ukristo. Paulo, aliyekuwa amekwisha kumuongoa Filemoni pia, aliamua kuwapatanisha kwa barua iliyomo sasa katika Agano Jipya.[6]).

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads