Mdudu-ute

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mdudu-ute
Remove ads

Wadudu-ute (faila Onychophora, Kiing. velvet worms) ni viumbehai vinavyofanana na nyungunyungu wafupi na wanene. Wana mnasaba na vidudu-dubu na arithropodi. Jina lao linarejea uwezo wao wa kurushia ute katika vitundu viwili vya matezi nyuma ya mdomo ili kujitetea au kukamata mawindo.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...

Mwili wa wadudu-ute umerefuka na una pingili nyingi. Kila pingili inabeba jozi ya miguu isipokuwa pingili tatu za kichwa. Tofauti na arithropodi miguu hiyo haina viungo lakini ni kama vifuko vilivyojaa na hemolimfi (“damu”). Inaweza kusogea kwa msaada wa musuli chini ya ngozi. Kichwa kinabeba vipapasio viwili kwenye pingili la kwanza, lakini hivi havina homolojia na vile vya arithropodi. Pingili ya pili lina kipenyo kinachofanya kazi ya mdomo lakini, tena, hiki hakina homolojia na mdomo wa arithropodi. Kuna mataya (mandibili) mawili yenye ncha kali katika mdomo. Vitundu vya matezi ya ute vipo kwenye pingili la tatu.

Ngozi ya wadudu-ute ina tabaka la nje la khitini na tabaka la ndani la seli. Chini ya ngozi kuna matabaka matatu ya musuli. Nje ya ngozi inabeba nywele fupi zinazokupa hisi ya mahameli (asili ya jina la Kiingereza velvet worm).

Remove ads

Spishi za Afrika

  • Opisthopatus amatolensis
  • Opisthopatus amaxhosa
  • Opisthopatus cinctipes
  • Opisthopatus drakensbergi
  • Opisthopatus herbertorum`
  • Opisthopatus highveldi
  • Opisthopatus kwazululandi
  • Opisthopatus laevis
  • Opisthopatus natalensis
  • Opisthopatus roseus
  • Opisthopatus swatii
  • Peripatopsis alba
  • Peripatopsis balfouri
  • Peripatopsis birgeri
  • Peripatopsis bolandi
  • Peripatopsis capensis
  • Peripatopsis cederbergiensis
  • Peripatopsis clavigera
  • Peripatopsis hamerae
  • Peripatopsis intermedia
  • Peripatopsis janni
  • Peripatopsis lawrencei
  • Peripatopsis leonina
  • Peripatopsis moseleyi
  • Peripatopsis overbergiensis
  • Peripatopsis purpureus
  • Peripatopsis sedgwicki
  • Peripatopsis stelliporata
  • Peripatopsis storchi
Makala hiyo kuhusu "Mdudu-ute" inatumia jina ambalo halijakuwepo kwa lugha ya Kiswahili. Jina hili linapendekezwa kwa jina la mnyama huyu au wanyama hawa amba(ye)(o) ha(wa)na jina kwa sasa.

Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili hazina jina kwa mnyama huyu au wanyama hawa.

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mdudu-ute kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads