Nge-mjeledi kibete

From Wikipedia, the free encyclopedia

Nge-mjeledi kibete
Remove ads

Nge-mjeledi vibete (kutoka Kiing. microwhip scorpion) ni arithropodi wa oda Palpigradi katika ngeli Arachnida wafananao na nge-mjeledi wadogo kabisa. Kwa kadiri urefu wao ni mm 1-1.5 na mm 3 ni urefu mkubwa kabisa. Kama arakinida wote wana miguu minane, lakini jozi ya kwanza imekuwa kama maungo ya hisi. Kwa upande mwingine pedipalpi hutumika kwa kutembea, kwa hivyo inaonekana kama wadudu hawa wana miguu kumi. Mjeledi wa jina lao ni aina ya mkia mrefu na mwembamba wenye manyoya; urefu wake uneweza kuwa sawa na urefu wa kiwiliwili. Kama kawaida kiwiliwili kina sehemu mbili: kefalotoraksi (cephalothorax: kichwa na kidari) na fumbatio. Nge-mjeledi vibete hawana macho na kwa kawaida hawana maungo ya kupumua; hupata oksijeni kupitia kutikula (“ngozi”) yao kwa ajili ya ukubwa wao mdogo sana. Lakini spishi kadhaa zina vifuko fumbationi vinavyofanana na mapafu. Wadudu hawa huishi katikati ya chembe za ardhi ambapo hula vijidudu na viani.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Spishi za Afrika

  • Allokoenenia afra
  • Eukoenenia angolensis
  • Eukoenenia ankaratrensis
  • Eukoenenia antanosa
  • Eukoenenia bara
  • Eukoenenia berlesei
  • Eukoenenia chartoni
  • Eukoenenia deceptrix
  • Eukoenenia delphini
  • Eukoenenia depilata
  • Eukoenenia fossati
  • Eukoenenia hesperia
  • Eukoenenia lauteli
  • Eukoenenia lawrencei
  • Eukoenenia machadoi
  • Eukoenenia maroccana
  • Eukoenenia meridiana
  • Eukoenenia necessaria
  • Eukoenenia sakalava
  • Eukoenenia trehai
  • Koeneniodes frondiger
  • Koeneniodes madecassus
  • Koeneniodes malagasorum
  • Triadokoenenia millotorum
Makala hii kuhusu "Nge-mjeledi kibete" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili microwhip scorpion kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni nge-mjeledi kibete.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads