Pansofi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Pansofi (alifariki 250 hivi) alikuwa Mkristo wa Misri ambaye aliteswa na hatimaye kufia dini yake wakati wa dhuluma ya kaisari Decius[1].

Maisha

Mtoto wa gavana wa Aleksandria, Misri, aliporithi mali ya baba yake, aliigawa yote kwa mafukara akaenda kuishi kama mkaapweke kwa miaka 20.

Sifa yake ya utakatifu ilimfanya akamatwe na kuuawa dhuluma mpya ilipoanza.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Januari.

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads