Parasitamoli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Paracetamol (pia inajulikana kama acetaminophen) ni dawa inayotumika kutibu maumivu na homa.[1][2] Dawa hii kawaida hutumiwa kupunguza maumivu ya chini hadi ya wastani.[1] Ushahidi umechanganyika kuhusiana na matumizi yake ili kupunguza homa kwa watoto.[3][4] Mara nyingi huuzwa pamoja na dawa zingine, kama vile dawa nyingi za baridi.[1] Paracetamol pia hutumiwa kwa maumivu makali, kama vile maumivu ya saratani na maumivu baada ya upasuaji, pamoja na dawa za maumivu ya afyuni.[5] Kwa kawaida, dawa hii hutumiwa ima kwa mdomo au kwa njia ya haja kubwa, lakini pia inapatikana kwa kudungwa sindano kwenye mshipa.[1][6] Madhara yake hudumu kati ya saa mbili hadi nne.[6]
Paracetamol kwa ujumla ni salama katika kipimo kilichopendekezwa.[7] Kiwango cha juu cha kila siku kilichopendekezwa kwa mtu mzima ni gramu tatu hadi nne.[8][9] Viwango vya juu vinaweza kusababisha sumu, pamoja na kushindwa kwa ini.[1] Upele mkubwa wa ngozi unaweza kutokea mara chache.[1] Inaonekana kuwa salama wakati wa ujauzito na wakati wa kunyonyesha.[1] Kwa wale walio na ugonjwa wa ini, bado inaweza kutumika, lakini kwa kipimo cha chini.[10] Imeainishwa kama dawa ya kutuliza maumivu.[6] Haina shughuli kubwa ya kupambana na mwasho.[11] Jinsi inavyofanya kazi sio wazi kabisa.[11]
Paracetamol ilitengenezwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1877.[12] Ni dawa inayotumika sana kwa maumivu na homa nchini Marekani na Ulaya.[13] Iko kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Ulimwenguni. [14] Paracetamol inapatikana kama dawa ya kawaida, na majina ya chapa ikiwa ni pamoja na Tylenol na Panadol miongoni mwa mengine. [15] Bei yake ya jumla katika nchi zinazoendelea ni chini ya US$0.01 kwa kila dozi.[16] Nchini Marekani, inagharimu takriban US$0.04 kwa kila dozi.[17] Mnamo mwaka wa 2017, ilikuwa dawa ya 25 inayoagizwa zaidi nchini Marekani, ikiwa na maagizo zaidi ya milioni ishirini na nne.[18] [19]
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads