Paulina Visintainer

From Wikipedia, the free encyclopedia

Paulina Visintainer
Remove ads

Paulina Visintainer (Vigolo Vattaro[1], leo nchini Italia, 16 Desemba 1865 - Ipiranga, Brazil, 8 Julai 1942) alikuwa bikira wa Italia kaskazini ambaye alihamia Brazil katika ujana wake akaanzisha huko shirika la Masista Wadogo wa Kukingiwa Dhambi ya Asili kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa na maskini.

Thumb
Mt. Paulina.

Baada ya matatizo mengi, alitumikia shirika hilo kwa unyenyekevu mkubwa na sala ya kudumu[2]

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 18 Oktoba 1991, halafu mtakatifu tarehe 19 Mei 2002.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 9 Julai[3][4].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads