Ponsyano Ngondwe

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Ponsyano Ngondwe (alifariki Ttaka Jiunge, 26 Mei 1886) alikuwa waziri wa Mwanga II (1884 - 1903). Bila kujali dhuluma iliyoanzishwa na mfalme huyo, alipata ubatizo na kwa ajili hiyo alifungwa mara; wakati wa kupelekwa kuuawa alichomwa njiani kwa mkuki [1].

Ni mfiadini mmojawapo kati ya Wakristo 22 wa Kanisa Katoliki wanaojulikana na kuheshimiwa duniani kote kama Wafiadini wa Uganda.

Hao walikuwa wahudumu wa ikulu ya kabaka wa Buganda ambao waliuawa kati ya tarehe 15 Novemba 1885 na tarehe 27 Januari 1887 kwa sababu ya kumwamini Yesu Kristo baada ya kuhubiriwa Injili na Wamisionari wa Afrika walioandaliwa na kardinali Charles Lavigerie.

Hawa ndio wafiadini wa kwanza wa Kusini kwa Sahara kuheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 3 Juni, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 26 Mei[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads