Provino

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Provino (pia: Probino; Provins, Ufaransa, karne ya 4 - Como, Italia Kaskazini, 420 BK) anakumbukwa kama askofu wa pili wa Como.

Rafiki wa Ambrosi wa Milano, alitumwa naye huko Como kumsaidia askofu Felisi katika juhudi za kukamilisha uenezi wa Ukristo kote Italia baada ya Kaisari Theodosi I kuufanya dini rasmi ya Dola la Roma[1].

Baada ya kifo cha Felisi akawa mwandamizi wake akapambana na Uario.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Machi[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads