Ravenna

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ravenna
Remove ads

Ravenna ni mji wa Italia katika mkoa wa Emilia-Romagna. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mnamo mwaka wa 2009, kuna wakazi wapatao 135.000 wanaoishi katika mji huu. Mji upo m 4 juu ya usawa wa bahari.

Thumb
Sehemu ya mji
Ukweli wa haraka Nchi, Mkoa ...

Ravenna ni mashuhuri duniani kwa majengo yake ya kale ambayo ni mifano bora wa sanaa ya Kikristo ya karne za 5 na 6 BK. Kuna majengo 8 ya Ravenna yaliyoingizwa katika orodha ya UNESCO ya urithi wa dunia.

Remove ads

Historia

Kati ya 402 hadi 476 Ravenna ilikuwa makao makuu ya kaisari na hivyo mji mkuu wa Dola la Roma la Magharibi. Baada ya mwisho wa utawala wa Kiroma katika magharibi iliendelea kuwa mji mkuu wa wafalme wa Kijerumaniki kama Odoaker na Theodoriki. Wagermanik walikuwa Wakristo wa dhehebu la Waariano lakini wakazi wenyeji wa mji walifuata Ukristo wa Kiorthodoksi. Baada ya Italia kurudishwa chini ya Dola la Roma la Mashariki mji ulikuwa makao makuu ya gavana mkuu wa Bizanti katika Italia hadi mwaka 751 ambako kabila la Kijerumaniki la Walangobardi lilitawala tayari sehemu kubwa za Italia ya Kaskazini lilivamia pia Ravenna. Wakati ule Walangobardi walikuwa Wakatoliki na katika miaka iliyofuata Wakristo wa Ravenna walikuwa chini ya usimamizi wa Papa wa Roma.

Remove ads

Urithi wa dunia

Majengo yaliyo maarufu leo yalijengwa katika karne hizi za Ravenna kuwa mji mkuu wa Italia. Makanisa yote yamepambwa kwa mozaiki nzuri ukutani.

  • Kanisa la San Vitale (karne ya 6)
  • Kaburi kwa malkia Galla Placidia (karne ya 5); ilijengwa kwa umbo la kanisa dogo; malkia haikuzikwa hapa bali mjini Roma lakini inaaminiwa ya kwamba malkia aliandaa jengo hili kuwa kaburi lake.
  • Kanisa la Sant’Apollinare Nuovo (karne ya 6); hii ilikuwa kanisa kwa ajili ya mfalme Theodoriki ambako ibada zilisheherekewa kufuatana na liturgia ya Waariano.
  • Kaburi la Theodoriki; lina paa yenye ilichongwa na , mit einem Natursteindach von rund elf Metern Durchmesser und einem Meter Dicke, das aus einem einzigen, aus Istrien stammenden Monolithen herausgemeißelt wurde.
  • Kanisa la Ubatizo la Waariano (karne ya 6)
  • Kanisa la Ubatizo la Waorthodoksi (karne ya 5), nördlich des Doms, auch Neonische Taufkapelle genannt, gilt unter den achteckigen antiken Bauwerken Ravennas als das älteste.
  • Kanisa la askofu (karne ya 6)
  • Kanisa la Sant’Apollinare in Classe
Remove ads

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads