Richard Dawkins

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Richard Dawkins (alizaliwa Nairobi, Kenya, 26 Machi 1941) ni mwanabiolojia wa mageuzi na mwandishi kutoka Uingereza. Amekuwa profesa katika Chuo Kikuu cha Oxford na mshirika wa New College. Dawkins anajulikana kwa kitabu chake The Selfish Gene kilichotoka mwaka 1976, ambacho kilieleza kuwa Jenetikia ndizo msingi wa mageuzi na ndipo alipoanzisha neno “meme” kwa kueleza jinsi mawazo na utamaduni huenea kama Jenetikia. Ameandika vitabu vingine vingi vya sayansi na dini, na amekuwa akihamasisha watu kuelewa sayansi kwa urahisi. Dawkins pia amepata tuzo nyingi kutokana na mchango wake katika uandishi na mawasiliano ya kisayansi.[1][2]

Remove ads

Historia

Baada ya kuhamia Uingereza alisoma zoolojia na kupata PhD mwaka 1966 chini ya Nikolaas Tinbergen. Dawkins alipata umaarufu kwa kitabu The Selfish Gene (1976), kilichotambulisha neno “meme,” na The Blind Watchmaker (1986), ambacho kilipinga hoja ya muumbaji. Mwaka 2006 aliandika The God Delusion, akisema Mungu hayupo na dini ni udanganyifu. Dawkins ni mkosoaji mkubwa wa imani ya uumbaji na dini. Ameanzisha taasisi ya kusaidia sayansi na ameandika vitabu vingi vilivyopata umaarufu duniani.[3][4][5][6][7]

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads