Roland Brown

Mwanasheria Mkuu wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia

Roland Brown
Remove ads

Roland Brown alikuwa Mwingereza wa kwanza kuhudumu kama Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Tanganyika iliyokuja kuwa sehemu ya Tanzania baadaye.[1]

Thumb
Brown wa pili kushoto akiwa na Mwalimu Nyerere

Maisha ya awali na taaluma

Brown alikuwa mkufunzi katika chuo cha Trinity College, Cambridge katika Chuo kikuu cha Cambridge, wakati wa harakati za uhuru wa Tanganyika; aliteuliwa kuwa mshauri mkuu wa Mwalimu Julius Nyerere.[2]

Tanzania

Mwaka 1961 aliteuliwa kuwa Mwanasheria mkuu wa kwanza baada ya uhuru wa Tanganyika.[3] Baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yaliyoangusha utawala wa kisultani, Brown aliteuliwa na Mwalimu Nyerere kuandaa hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.[4]

Mwaka 1965 alimaliza muda wake na nafasi yake ikachukuliwa na Mark Bomani.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads