Rula

kifaa kinachotumika kupima urefu. Kizio cha kawaida cha kupima urefu ni Mita (m). From Wikipedia, the free encyclopedia

Rula
Remove ads

Rula (kutoka Kiingereza ruler) ni kifaa kinachotumika kupima urefu. Kizio cha kawaida cha kupima urefu ni Mita (m).

Thumb
Picha ya kifaa kiitwacho rula.

Hata hivyo, mita si kizio pekee cha kupima urefu, kuna vizio vingine kama vile Kilometa, sentimeta, Milimita na vilevile Maili n.k. ambayo hutumika kupika urefu.

Aina

Rula hutengenezwa kwa aina mbalimbali na urefu tofauti. Baadhi ni za mbao, chuma au plastiki. Rula fupi ni bora kwa kuweka mfukoni, wakati nyingine ni ndefu kwa matumizi mbalimbali.

Historia

Thumb
Rula ya mbao ya seremala na zana nyingine zilizopatikana karne ya 16.

Rula zilianza kutumika miaka mingi iliyopita. Ufito wa shaba wa kupimia wa kale kabisa ni wa mwaka 2650 KK na ulivumbuliwa na Mjerumani Eckhard Unger huko Nippur.

Rula zilizotengenezwa kwa pembe ya ndovu zilitumiwa kwenye Ustaarabu wa Bonde la Indus kabla ya 1500 KK. Rula ya aina hii ilipatikana wakati wa uchimbaji huko Lothal (2400 KK) ikiwa na milimita 1.6.

Anton Ullrich alivumbua rula ya kukunja mwaka 1851. Frank Hunt alivumbua rula inayopindika mwaka 1902.[1]

Remove ads

Faida za rula

1) hutumika kupima urefu wa kitu

2) hutumika katika kuchora

Marejeo

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads