Useremala
From Wikipedia, the free encyclopedia
Useremala (kutoka neno la Kiajemi na la Kiarabu) ni aina ya ufundi ambao kimapokeo uilitegemea mbao, lakini siku hizi hata vitu vingine kama metali hutumika[1]. [2].





Seremala hutengeneza vitu mbalimbali kama vile masanduku ya kumwagia zege, milango na madirisha na fremu zake, samani, makabati n.k.
Mara nyingi mtu anajifunza kazi hiyo kwa kusaidia seremala stadi, lakini siku hizi kuna vyuo vingi vinavyofundisha fani hiyo.
Hata upande wa vifaa, badala ya vile vinavyotegemea nguvu ya mikono kama randa, siku hizi wengi wanatumia mashine kama msumeno wa mnyororo maalumu ya kuchania, kunyoosha, kupogoa, kurandia n.k.
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.