Salamu Maria

From Wikipedia, the free encyclopedia

Salamu Maria
Remove ads

Salamu Maria (kwa Kilatini Ave Maria) kwa asili ni sala ya Wakatoliki wa Kanisa la Kilatini ambayo inamsifu Bikira Maria na kumuomba sala zake hadi saa ya kufa.

Thumb
Kupasha Habari, kadiri ya Fra Angelico.

Sala hiyo imeenea hata kwa Wakristo wengine, hasa Waanglikana, lakini kwa namna tofauti inatumiwa pia katika Ukristo wa Mashariki.

Hii ni kwa sababu sehemu kubwa ya sala hiyo inatokana na Injili (Lk 1:28,42) moja kwa moja:

  • Χαῖρε, κεχαριτωμένη, ὁ Κύριος μετὰ σοῦ / Chaire, kecharitōmenē, o Kyrios meta sou / Salamu uliyejaa neema, Bwana yu nawe (maneno ya Malaika Gabrieli)
  • Εὐλογημένη σὺ ἐν γυναιξὶν καὶ εὐλογημένος ὁ καρπὸς τῆς κοιλίας σου / eulogēmenē su en gynaixin kai eulogēmenos o karpos tēs koilias sou / Umebarikiwa wewe kati ya wanawake na umebarikiwa mzao wa tumbo lako (maneno ya Elizabeti)

Katikati ya karne ya 13 sala ilikuwa inaundwa na maneno hayo tu pamoja na kuingiza jina la Maria, inavyoonekana katika ufafanuzi wa Thoma wa Akwino.[1]

Mwishoni mwa karne ya 15 yaliongezwa maneno ya kumuomba Maria sala zake.[2]

Hatimaye sala kwa Kilatini imekuwa hivi:

Áve María, grátia pléna,
Dóminus técum.
Benedícta tu in muliéribus,
et benedíctus frúctus véntris túi, Iésus.[3]
Sáncta María, Máter Déi,
óra pro nóbis peccatóribus,
nunc et in hóra mórtis nóstrae. Ámen.

Tafsiri ya Kiswahili ni:

Salamu María, umejaa neema,
Bwana yu nawe.
Umebarikiwa kuliko wanawake wote,
na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa.
Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu,
utuombee sisi wakosefu,
sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
Remove ads

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads