Santilya
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Santilya ni kata ya Wilaya ya Mbeya Vijijini katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Ipo katika tarafa ya Isangati ikiwa na vijiji kama Itizi, Sanje, Jojo, Iswago, Nsheha, Idunda n.k. Imepakana na kata ya Isuto, ikiwa upande wa magharibi, Ilembo upande wa kusini, Igale upande wa mashariki, kaskazini ni wilaya ya Ileje.
Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 17,624 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 17,578 [2] walioishi humo.
Santilya ni kitovu cha Umalila na wakazi asilia ni hasa Wamalila. Lugha yao ni Kimalila. Kata ya Santilya ina koo kubwa ambazo ni Mwaluanda ambao ni machifu, pia kuna koo kama Mwangwale, Wapyambala, Mwamahonje, Mwasile, Mwasenga, Ngoya n.k. Wamalila ni wakarimu na wachapakazi.
Wakazi wa Santilya wanajihusisha na kilimo cha viazi mviringo na vitamu, maharagwe, mahindi na pareto ambalo ni zao la biashara.
Upande wa elimu Wamalila hawakuwa na mwamko mwanzo ingawa sasa wanaonekana kuja kwa kasi. Kuna shule ya sekondari.
Katika mazingira ya Santilya Jeshi la Wokovu lina wafuasi wengi kiasi.
Msimbo wa posta ni 53211.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads