Milima ya Sayan

From Wikipedia, the free encyclopedia

Milima ya Sayan
Remove ads

Milima ya Sayan ni safu ya milima kusini mwa Siberia, Urusi, hasa kwenye Jamhuri ya Tuva, na kaskazini mwa Mongolia . Hapo zamani milima ilikuwa mpaka kati ya Mongolia na Urusi. [1]

Thumb
Ziwa la "Mapepo ya milima"
Sayan Magharibi

Vilele vya Milima ya Sayan na maziwa baridi kati yake ni chanzo cha matawimito yanayounda mto Yenisei, unaoanza hapa na kuendelea kwa zaidi ya kilomita 3000 hadi Bahari ya Aktiki. Hili ni eneo lililotengwa kwa miaka mingi, kwa kuwa limefungwa na Umoja wa Kisovyeti tangu mwaka 1944. [2]

Thumb
Mlima Mönkh Saridag.

Sayan Mashariki inaenea kwa km 1,000 kutoka mto Yenisei hadi Ziwa Baikal. Sayan Magharibi inaendeleza Milima ya Altai, ikienea kwa km 500 kutoka longitudo ya 89° hadi katikati ya Mashariki.

Wakati mwinuko wa wastani ni mita 2,000 hadi 2,700, vilele vya miamba migumu kama itale hufikia zaidi ya mita 3,000. Kilele cha juu kabisa ni Mönkh Saridag chenye kimo cha mita 3,492.

Remove ads

Vidokezo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads