Scipio Africanus
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Publius Cornelius Scipio Africanus (236–183 KK) [1] alikuwa kiongozi wa kijeshi wa Jamhuri ya Roma na mwanasiasa wakati wa vita ya pili dhidi ya Karthago. Anakumbukwa hasa kwa uongozi wake katika mapambano ya kumshinda Hanibal wa Karthago.
Scipio alishinda mapigano ya Zama katika Afrika ya Kaskazini. Jina lake Africanus (Mwafrika) limetokana na mahali pa ushindi wake, si kutokana na kuzaliwa huko, wala kuwa na ukoo wa Kiafrika. Kutokana na ushindi dhidi ya mpinzani aliyekuwa hatari kuu kwa Roma ya Kale Scipio alikuwa kati ya viongozi wa kijeshi mashuhuri zaidi katika historia ya Dola la Roma. Baada ya mapigano ya Zama Karthago ilipaswa kuomba amani ikapewa masharti ya fedheha.
Remove ads
Marejeo
Vitabu
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads