Selulitisi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Selulitisi (kutoka Kilatini na Kiingereza: "cellulitis") ni ugonjwa unaotokana na bakteria unaoathiri undani wa ngozi.
Dalili zake ni pamoja na ngozi kubadilika rangi kuwa nyekundu na pia kuvimba. Sehemu iliyoathiriwa huwa na maumivu. [1]
Mgonjwa anaweza kuwa na homa na kujisikia mchovu.[2]
Miguu na uso ndio sehemu zinazoathiriwa zaidi na ugonjwa huu ingawa unaweza kuathiri sehemu yoyote ya mwili.
Kati ya sababu zinazofanya mtu kupata ugonjwa huu ni pamoja na unene kupita kiasi, kuvimba kwa miguu, na uzee. Bakteria wanaosababisha ugonjwa huu ni streptococci na Staphylococcus aureus.
Matibabu yake huwa ni kwa dawa kama vile cephalexin, amoxicillin au cloxacillin. Kwa wale wenye matatizo ya kutumia dawa kama penicillin, dawa za erythromycin na clindamycin hutumiwa.
Wengi sana wanapona bada ya siku 7-10 za kutumia dawa kama hizo.
Remove ads
Picha
- Mkono ulioathiriwa.
- Mguu ulioathiriwa na mguu ambao haujaathiriwa.
- Mguu ulioathiriwa hadi kwenye unyayo.
Marejeo
Soma zaidi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads