Serati

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Serati (pia: Cerat, Ciratus, Ceretius, Ceratus, Ceras, Gerase; alifariki 450 hivi) alikuwa askofu wa Grenoble katika Burgundy, leo nchini Ufaransa, kwa miaka kumi, akidumisha imani sahihi kati ya waumini wake dhidi ya Uario wa wavamizi wa nchi ile [1].

Ukweli wa haraka Nchi, Kazi yake ...

Kutokana na msimamo huo, alimshukuru Papa Leo I kwa barua aliyomtumia Patriarki Flaviani wa Konstantinopoli.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Heshima hiyo ilithibitishwa na Papa Pius X tarehe 9 Desemba 1903.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Juni.[2]

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads