Shaaban (mwezi)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Shaaban (kwa Kiarabu: شعبان, sha‘bān) ni mwezi wa nane katika kalenda ya Kiislamu. Inafuata Rajabu ikifuatwa na Ramadan.

Ilhali ni mwezi kabla ya Ramadani ni pia wakati ambako mwanzo wa saumu unatangazwa.[1]

Nisfu Shaaban

Siku ya 15 ya Shaaban inajulikana kama "usiku wa kumbukumbu" au Laylatul Bara-at [2] lakini adhimisho hilo lina utata.[3]. Kufuatana na hadith Mtume Muhammad alitaja tarehe hiyo kuwa siku maalumu, hivyo kuna Waislamu wanaoamini ya kwamba usiku huo una baraka za pekee. Wengine hukaa usiku huo pamoja wakisoma Korani na kushiriki katika sala za pekee. Wengine wanapinga ibada hizo.[4]

Sikikuu ya Imamu Mahdi

Washia Ithna ashari husheherekea tarehe 15 Shaaban kama sikukuu ya kuzaliwa kwa imamu wao wa 12 na wa mwisho, Muhammad al Mahdi.[5]

Tarehe zake

Ilhali kalenda ya Kiislamu ni kalenda ya mwezi miezi yake huanza wakati wa kutazamwa kwa hilali ya mwezi mpya. Pia kwa sababu mwaka wa mwezi ni mfupi kuliko mwaka wa jua basi tarehe za Shaaban zinapita kwenye majira. Tarehe zake kwa miaka ya karibu ni takriban[6]:

Maelezo zaidi Mwaka baada ya Hijra, Siku yake ya kwanza katika kalenda ya BH / AD) ...

Kumbukumbu maalumu

  • 01 Shaaban, kuzaliwa kwa Zainab bint Ali
  • 03 Shaaban, kuzaliwa kwa Hussein ibn Ali
  • 04 Shaaban, kuzaliwa kwa Abbas ibn Ali
  • 05 Shaaban, kuzaliwa kwa Ali ibn Hussein
  • 07 Shaaban, kuzaliwa kwa Qasim ibn Hasan
  • 11 Shaaban, kuzaliwa kwa Ali al-Akbar ibn Husayn
  • 11 Shaaban 1293 BH, Abdulhamid II alikuwa sultani wa Milki ya Osmani
  • 15 Shaaban, sikukuu ya Laylat al-Bara'at au Nusu Shaaban; kuzaliwa kwa Muhammad al-Mahdi
Remove ads

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads