Hussein ibn Ali

From Wikipedia, the free encyclopedia

Hussein ibn Ali
Remove ads

Hussein ibn Ali[1] (kwa Kiarabu: حسين بن علي‎; 11 au 13 Januari 626 BK10 Oktoba 680 BK, sawa na 3 Shaabani 4 BH - 10 Muharram 61 BH; 3 شعبان 4 هـ - 10 محرم 61 هـ) alikuwa mjukuu wa Mtume Muhammad akitazamwa kama imamu wa kwanza wa Washia. Alizaliwa mjini Makka, baba yake alikuwa Ali ibn Abi Talib (khalifa wa nne na mama yake Fatimah Zahra binti Muhammad. Kaka yake alikuwa Hasan ibn Ali imamu wa pili wa Washia.

Thumb
Msikiti wa Kaburi la Imamu Hussein mjini Karbala.
Thumb
Taswira ya Kiajemi inayomwonyesha Hussein katika mapigano ya Karbala.

Aliuawa katika Mapigano ya Karbala pamoja na wengi wa familia yake kwenye siku ya Ashura. Hivyo anatazamwa kama mfiadini, hasa kati ya Washia, na kukumbukwa kwenye sherehe za mwezi Muharram, hasa siku za Tasua na Ashura.[2]

Hussein ibn Ali ni muhimu sana kati ya Washia wanaomwangalia kama mtu mtakatifu kutokana na uhusiano wake wa karibu na mtume Muhammad na kama kielelezo kwa ushujaa katika mapigano ya Karbala. Washia wanamkumbuka na kukumsifu kwa upinzani wake dhidi ya Yazid I aliyekuwa khalifa wa Wamuawiya.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads