Shikamoo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Shikamoo ni neno linalotumiwa kumsabahi mtu. Maana ya neno hilo huelezwa kuwa kifupi cha "niko chini ya mguu wako" kama tamko la heshima mbele ya mkubwa. Hivyo ni salamu inayotumiwa na wadogo kwa wale wanaowazidi umri, hasa wazee. La sivyo, salamu kama "habari za sasa hivi" hutumika [1].

Jibu lake ni "Marahaba", salamu inayotumiwa kati ya Waarabu kwa maana ya "sawa kabisa", ila kwa matamshi ya "marhaba". Maana asili ya neno hilo ni "Mungu akupe nafasi", na jibu ni "marhabteen" yaani marhaba mara mbili.

Matumizi yake ni kawaida katika Kiswahili nchini Tanzania, kumbe huko Kenya mara nyingi haieleweki isipokuwa kwenye maeneo ya pwani[2].

Inasemekana pia neno lenyewe lilitumiwa na Waarabu katika biashara ya watumwa na utumwa kama amri kwa watumwa yenye maneno mawili ambayo ni: "shika" na "moo" likimaanisha "miguu". Hivyo shikamoo ilimaanisha shika miguu (yangu); na baada ya mtumwa kutii amri hiyo kwa kushika miguu ya mhusika, kwa mara nyingine tena mhusika alikubali kushikwa na kuitikia "marhaba".

Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads