Shtuko la moyo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Shtuko la moyo
Remove ads

Shtuko la moyo (kwa Kiingereza acute myocardial infarction au heart attack) linatokea pale ambapo ghafla mshipa wa damu ndani ya moyo unaziba. Mishipa ya namna hiyo inasafirisha damu na oksijeni. Mshipa mmojawapo moyoni ukiziba, damu haiwezi tena kufikia sehemu ya moyo, na hivyo sehemu hiyo inakuja kukosa oksijeni. Tukio hilo linaitwa iskemia (kwa Kiingerez: ischaemia), nalo mara nyingi linasababisha maumivu kifuani (angina pectoris). Ikiwa iskemia inadumu kirefu, msuli wa moyo unakufa kwa kukosa oksijeni (infarction).

Thumb
Maumivu kifuani; nyekundu iliyokolea: sehemu za kawaida zaidi, nyekundu isiyokolea: sehemu nyingine zinazoweza kupatwa.
Thumb
Maumivu mgongoni.

Shtuko la moyo ni hatari kubwa inayodai msaada wa daktari, lakini dakika za kwanza ndizo muhimu zaidi kwa kuokoa uhai wa mgonjwa wa namna hiyo. Kumbe wengi wanasubiri masaa.[1]

Baadhi ya madhara yanayotokana na shtuko hilo yanaweza kurekebishwa ikiwa mhusika anatibiwa saa za kwanzakwanza.

Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads