Sienna Guillory
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Sienna Tiggy Guillory (amezaliwa tar. 16 Machi 1975) ni mwigizaji wa filamu, tamthilia, na mwanamitindo wa Kiingereza. Mara nyingi alifanya kazi za uanamitindo mbali kidogo na sanaa ya uigizaji. Pia anafahamika zaidi kwa kuigiza kama Jill Valentine katika filamu ya Resident Evil: Apocalypse na kucheza tena kama Elf Arya Drottningu katika filamu ya Eragon.
Huyu ni binti wa mzee Isaac Guillory, mpiga gitaa Mwiingereza-Mkuba. Guillory amepata kuigiza katika filamu nyingi za Kiingereza, na kisha baadaye filamu za Kiamerika. Si muda mrefu sana, amepata kucheza katika filamu za uzushi wa kisayansi na za kifantasia, ambazo zilitungwa kwa ajili ya vijana/watoto.
Remove ads
Maisha
Mahusiano
Guillory alianza kutembea na mwigizaji mwenzake Nick Moran kunako mwaka wa 1997. Wawili hao walikuja kuachana baada ya miaka mitatu, yaani kunako mwaka wa 2000. Mwaka huohuo baadaye, akaanza kutembea na Enzo Cilenti. Cilenti na Guillory walioana kunako mwaka wa 2002, na wakati sherehe za ndoa yao Guillory alivaa gauni ya harusi la bibi yake.[1][2] Wawili hao wanaishi mjini Los Angeles na London, lakini kunako mwaka wa 2007, wanandoa hao wakaamua kuweka makazi yao rasmi mjini Los Angeles.[3]
Remove ads
Filamu alizocheza
Filamu za kawaida
Televisheni
Remove ads
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads