Sirige

From Wikipedia, the free encyclopedia

Sirige
Remove ads

Sirige ni aina ya barakoa inayotumika katika ngoma za kimila za Wadogon wa Mali.

Thumb

Barakoa hii inatambulika kwa urefu wake ambao unaweza kuwa kutoka mita 4 hadi 6[1].

Ina mashimo mawili zinazokwenda sambamba kutoka juu hadi chini. Pia inatumia miundo ya pembetatu kuifanya iwe maridadi. Rangi yake kuu ni nyeusi na nyeupe, lakini rangi nyingine pia zinaweza kutumika.

Mistari ya mshazari iliyo kwenye barakoa hii inaonyesha jinsi asili ya maisha duniani imeshikamana. Inavyochezeshwa mbele na nyuma huonyesha jinsi mchana na usiku hupita. Rangi nyekundu iliyo kwenye mavazi ya rapia humaanisha hedhi ya mwanamke[2].

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads