Suleiman I

From Wikipedia, the free encyclopedia

Suleiman I
Remove ads

Suleiman I (kwa Kituruki: سلطان سليمان اول, Sultān Suleimān-i evvel au قانونى سلطان سليمان‎, Kānūnī Sultān Suleimān; 6 Novemba 14945 Septemba/6 Septemba 1566) alikuwa sultani wa 10 wa Milki ya Osmani. Alitawala miaka 46 kuanzia 1520 hadi 1566. Hakuna sultani mwingine aliyekaa muda mrefu kama yeye. Watu wa magharibi walimwita "Suleimani Mwadhimu"; katika dunia ya Kiislamu alijulikana kama [1] "Suleimani Kanuni" kutokana na muundo wa sheria alizorekebisha na kuunda.

Ukweli wa haraka Sultani wa Milki ya Osmani, Tarehe za utawala ...

Wakati wa karne ya 16 Suleimani alikuwa mtawala mashuhuri aliyeongoza milki yake hadi kufikia kwenye kilele cha uwezo na uenezaji wake. Suleimani mwenyewe aliongoza jeshi lake kuteka maboma ya Wakristo kama Belgrad, Rhodos na sehemu kubwa ya Hungaria hadi Vienna alipopaswa kurudi nyuma.

Vilevile aliteka sehemu kubwa za Mashariki ya Kati pamoja na Uajemi ya magharibi katika vita zake dhidi ya watawala Wasafawi. Afrika ya Kaskazini aliweka chini ya utawala wake hadi Algeria. Jeshi la maji la Waosmani lilitawala Mediteranea, Bahari ya Shamu na Ghuba ya Uajemi. Katika bahari Hindi Waosmani walipagana na Wareno na kutuma wanmajeshi hadi Aceh katika Indonesia.

Remove ads

Marejeo

Marejeo

Soma pia

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads