Ghuba ya Uajemi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ghuba ya Uajemi (Kiajemi: خلیج فارس khalij-e fārs; Kiarabu: الخليج الفارسي al-khalīj al-fārsī; pia: الخليج العربي al-khalīj al-ʿarabī „Ghuba Arabu“) ni ghuba kubwa ya Bahari Hindi kati ya Irani na rasi ya Uarabuni.

Inaanza kwenye Mlango wa Hormuz na kuendelea hadi mwisho wake upande wa Kuwait na mdomo wa Shatt al Arab.
Ni kawaida kuiita ghuba ya Uajemi lakini katika fitina ya miaka iliyopita nchi kadhaa za Waarabu ziliiita "Ghuba Arabu". Zamani iliitwa pia "Ghuba ya Basra" na hili ndilo jina lake hadi leo katika lugha ya Kituruki "Basra Körfezi.
Remove ads
Jiografia
Eneo lote la ghuba ni km² 233,000. Maji matamu huingia kwa njia ya mito ya Frati na Hidekeli inayounganika katika Shatt al Arab.
Urefu wake ni takriban km 1,000 na upana wake kati ya km 200 na 300. Kina hakizidi m 100.
Mlango wa Hormuz unaunganisha ghuba hiyo na Bahari Arabu ambayo ni bahari ya kando ya Bahari Hindi.
Nchi jirani
Nchi zinazopakana na ghuba ni:
Umuhimu wa kisiasa na wa kiuchumi
Nchi za ghuba zimekuwa muhimu sana duniani kwa sababu ya mafuta ya petroli inayopatikana huko kwa wingi. Utajiri huo umebadilisha sura ya nchi zinazopakana na ghuba, lakini umesababisha pia vita kadhaa kama vile vita ya Irani-Iraki, vita ya Iraki-Kuwait, vita ya ghuba.
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ghuba ya Uajemi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads