Sulfuri
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Sulfuri (pia salfa au kibiriti, ing. sulfur) ni elementi simetali yenye namba atomia 16 kwenye mfumo radidia na uzani atomia 32.065. Alama yake ni S. Kwenye hali sanifu ni imara kuwa fuwele zenye rangi ya njano.
Remove ads
Kutokea duniani
Hutokea duniani kama elementi tupu hasa kwenye volkeno, lakini zaidi kwenye kampaundi ndani ya madini ya sulfidi. Leo hii inapatikana kutokana na mafuta ya petroli wakati yakisafishwa.
Sulfuri ni elementi ya lazima kwa maada hai na seli zote zinatumia sulfuri.
Matumizi ya kibiashara
Matumizi yake ya kiuchumi ni hasa kwa mbolea ya chumvi, lakini pia katika baruti, viberiti na dawa za kuulia wadudu.
Sulfuri - kibiriti
Jina jingine la sulfuri ni "kibiriti" (kutoka Kiarabu كبريت) linalopatikana kwa mfano katika tafsiri za Biblia (k.m. Luka 17,29, Ufunuo 9,17). Matumizi ya neno hilo kwa ajili ya "vibiriti" yalijitokeza kwa sababu mwanzoni kichwa cha vijiti kilikuwa na mchanganyiko wa dawa zenye sulfuri au "kibiriti" ndani yake. Hivyo tafsiri nyingine ya "vibiriti" ni "vijiti vyenye sulfuri".
Viungo vya Nje
Tazama pia
- Mfumo radidia
- Orodha ya elementi
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sulfuri kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads