Sumo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Sumo (相撲, sumō) ni michezo ya miereka kutoka nchini Japani.[1]
Katika Sumo ni wapiganaji wawili (wanaitwa rikishi) wanaoshindana wakiangaliwa na refa. Mashindano hutekelezwa katika mviringo wenye kipenyo cha mita 4.55.
Kila mpiganaji analenga ama kumsukuma mwenzake nje ya mviringo, au kumlazimisha kugusa sakafu na sehemu yoyote ya mwili wake isipokuwa nyayo.
Kila mwaka kuna mashindano (basho) makubwa yanayotekelezwa katika miji hufanyika Tokyo, Osaka, Nagoya na Fukuoka. Idadi ni mashindano 6 makuu ya kitaalamu (inayojulikana kama honbasho) kwa mwaka, kwenye miezi ya Januari, Machi, Mei, Julai, Septemba na Novemba.
Mashindano kawaida hudumu kwa siku 15 na huonyesha mechi kutoka kwa migawanyiko tofauti. Nafasi 5 za juu zinajulikana kama "Mgawanyiko wa Juu", pia huitwa Makuuchi (幕 内) au Makunouchi (幕 の 内). Kila shindano huwa na rikishi 42.
Remove ads
Wale ambao wamepata kiwango cha juu zaidi ni mabingwa wakuu (yokuzuna). [2]
- Akashi, karne ya 16 [2]
- Maruyama, (1712-1749)
- Tanikaze (Kajinosuke, 1750-1795)
- Onagawa (1758-1805)
- Ao no Matsu (1791-1851)
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads