Syr Darya

From Wikipedia, the free encyclopedia

Syr Darya
Remove ads

Syr Darya (kwa Kigiriki cha Kale ilijulikana kama Ἰαξάρτης, Iaxartes), ni mto wa Asia ya Kati.

Ukweli wa haraka
Thumb
Picha ya mto Syr Darya iliyopigwa kutoka anga-nje.

Chanzo cha maji yake kipo katika Milima ya Tian Shan huko Kirgizia na mashariki mwa Uzbekistan. Mto wenyewe unaanza Kirgizia katika bonde la Ferghana ambako matawimto mikubwa ya Naryn na Kara Darya inaungana. Unaendelea kupita kwa km 2,212 katika Tajikistan, Uzbekistan na Kazakhstan hadi kuishia katika Ziwa Aral.

Pamoja na Amu Darya ni mmoja kati ya mito mikubwa kwenye beseni la Ziwa Aral. Wakati wa utawala wa Umoja wa Kisovyeti maji ya mito hiyo miwili yalitumiwa kwa miradi mikubwa ya umwagiliaji iliyosababisha kukauka kwa asilimia 90 za Ziwa Aral.

Remove ads

Marejeo

Viungo va Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads