Tabaka (jamii)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Tabaka (jamii)
Remove ads

Tabaka katika jamii ni kundi la watu linalotofautiana na mengine kwa hali ya elimu, mali au asili. Tofauti kati ya matabaka zinaweza kuwa kubwa mno na kusababisha utovu wa haki.

Thumb
Matabaka matatu ya Ulaya kabla ya Mapinduzi ya Kifaransa: mkulima akibeba watu wa matabaka ya juu.

Hasa huko India, mtu aliyezaliwa katika tabaka fulani hawezi kupanda chati, hata kama akitajirika, tena watoto wake wataendelea kuhesabiwa wa tabaka hilohilo la mababu wao.

Katika nchi nyingi, matabaka yanategemea hasa uchumi, hivyo kila mtu anaweza kupanda na vilevile kushuka, hata ghafla[1][2].

Pengine wanatofautishwa:

  1. Mabwanyenye, yaani matajiri wa kupindukia
  2. Walala heri, yaani wenye kipato cha kati
  3. Walala hai, yaani wenye chakula cha kutosha, lakini si zaidi
  4. Walala hoi, yaani maskini
  5. Fukara/hohehahe, yaani maskini wa kupindukia
Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads