Chati
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Chati (kutoka ing. chart[1]) za data au jedwali, ambapo taarifa inawakilishwa na michoro ya aina mbalimbali. Chati inaweza kuwakilisha takwimu za data za simu, kazi au aina fulani za muundo wa ubora na hutoa maelezo tofauti.

Neno chati kama uwakilishi wa takwimu ya data ina maana nyingi:
Chati ya data ni aina ya mchoro au grafu, ambayo hupanga na inawakilisha tarakimu.
Ramani ambazo huwa na maelezo ya ziada kwa madhumuni maalum mara nyingi hujulikana pia kama chati, kama ramani za mabaharia na wanaanga.
Wakati mwingine michoro ya kodi za msingi za muziki huitwa chati au chati ya rekodi maarufu za muziki.
Kawaida chati hutumika kurahisisha uelewaji wa data kubwa na uhusiano kati ya sehemu za data hizo. Kawaida zinaweza kusomwa kwa haraka zaidi. Zinatumika katika nyanja mbalimbali kama vile sayansi na hesabu [2], biashara [3], n.k. na zinaweza kuchorwa kwa mkono (mara nyingi kwenye karatasi ya grafu) au kwa kompyuta kwa kutumia programu maalumu ya chati.
Aina fulani za chati ni bora zaidi kwa kuwasilisha data kuliko nyingine. Kwa mfano, data inayowakilisha namba zinazobadilika kwa kipindi cha muda (kama vile "mapato ya kila mwaka kutoka 1990 hadi 2000") zinaweza kuonyeshwa kwa ubora zaidi kwa kutumia chati ya mstari.
Remove ads
Aina za chati
Chati nne zinazotumika kwa wingi
- Histogram
- Bar chart
- Pie chart
- Line chart
Chati zisizotumika kwa wingi
- Bubble chart
- Polar area diagram
- Waterfall chart
- Radar chart
- Tree map
- Streamgraph
- GapChart
Chati maarufu zilizopewa majina
- Gantt chart
- Nolan chart
- PERT chart
- Smith chart
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads