Tandu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Tandu ni aina za arithropodi wembamba na warefu katika ngeli Chilopoda ya nusufaila Myriapoda wenye miguu mingi. Wanafanana kijuujuu na majongoo lakini hawa huenda polepole na hula dutu ya viumbehai, viani na kuvu. Tandu huenda mbio na hula wanyama wengine (invertebrati na vertebrati). Hata kama tandu huitwa centipedes (miguu mia) kwa Kiingereza na majongoo huitwa millipedes (miguu elfu), kwa ukweli wana kwa kadiri nambari sawa ya miguu: tandu wana miguu 16 hadi 300 na majongoo 36 hadi 750.
Remove ads
Spishi kadhaa za Afrika
- Lithobius variegatus, Tandu Milia (Common banded centipede)
- Pachymerium ferrugineum, Tandu Mwekundu (Pachymerium ferrugineum)
- Scolopendra abnormis, Tandu wa Kisiwa cha Nyoka (Serpent Island centipede)
- Scolopendra cingulata, Tandu Milia wa Mediteranea (Mediterranean banded centipede)
- Scolopendra morsitans, Tandu Kichwa-chekundu (Red-headed centipede au Tanzanian blue ringleg)
- Scutigera coleoptatra, Tandu wa Nyumbani (House centipede)
Remove ads
Picha
- Tandu milia
- Tandu milia wa Mediteranea
- Tandu wa nyumbani
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads