Teofilo wa Antiokia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Teofilo wa Antiokia (kwa Kigiriki Θεόφιλος ὁ Ἀντιοχεύς, Theofilos o Antiokheus, alifariki 183/185 BK) alikuwa askofu wa 7 wa Antiokia[1] baada ya Eros na kabla ya Masimo I[2][3].

Kutoka maandishi yake (Eusebi wa Kaisarea na Jeromu walitaja vitabu mbalimbali vya Teofilo vilivyokuwepo nyakati zao, ambavyo kati yake kimebaki kile Utetezi kwa Autolycus[4], rafiki yake msomi lakini Mpagani) tunajua kwamba alizaliwa na Wapagani katika eneo la kati ya mito Tigri na Eufrate, na kwamba aliingia Kanisa kwa kupendezwa na maadili ya Wakristo na kwa kusoma Biblia, hasa vitabu vya kinabii.[5]
Kutoka kwa mwanahistoria Eusebius wa Kaisarea tunajua juhudi zake za kutetea imani sahihi na kupinga uzushi, hasa ule wa Marcion[6][7], akichangia fasihi ya Kikristo, hoja za dini, ufafanuzi wa Biblia na utetezi wa dini kwa kutumia elimu yake pana.[8]
Maandishi yake ndiyo ya zamani kuliko yale yote tuliyonayo yanayotaja Utatu Mtakatifu.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads