Tmk Wanaume

From Wikipedia, the free encyclopedia

Tmk Wanaume
Remove ads

TMK Wanaume Family ni kundi la muziki wa kizazi kipya kutoka Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam Tanzania. Kundi lilianzishwa rasmi mnamo Septemba 16 mwaka 2002 mjini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa albamu ya Juma Nature iitwayo Ugali na hadi sasa limejijengea umaarufu katika albamu zake mbili ilizotoa ambazo ni Kutokea Kiumeni na Ndio Zetu. Wasanii wa kundi baadhi kabla ya wengine kujiengua ni Juma Nature, KR, Doro, D Chief, Mh Temba, Mzimu, Luteni Karama, Chege, Yp, Y Dash, na wengineo, halafu baada ya kutengana kukawa na "Tmk Wanaume Halisi" na Tmk Wanaume. Tmk Wanaume kiongozi wa kundi ni Mh Temba na Chege wakati Tmk Wanaume Halisi kiongozi wa kundi ni Juma Nature na Inspector Haroun.[1]

Thumb
Hii ni Kasha ya Albamu ya Tmk Wanaume Enzi Hizo Hawaja Sambaratika
Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads