Juma Nature
mwanamuziki wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Juma Kassim Ally, anayejulikana zaidi kama Juma Nature au Sir Nature (alizaliwa Dar es Salaam mwaka 1980), ni mwanamuziki wa aina ya Bongo Flava na Hip Hop kutoka Tanzania. Ni mwanzilishi wa kundi maarufu la TMK Wanaume Family.
Remove ads
Juma Nature ni msanii mbunifu ambaye si mtunzi wa mashairi tu, bali pia ana kipaji cha kipekee kinachochangiwa na sauti yake nzuri ya uimbaji. Moja ya sababu zinazoufanya muziki wake kupendwa sana Afrika Mashariki ni mashairi yake yenye maana na ujumbe wa kina. Miongoni mwa nyimbo zake zilizompa heshima kubwa kitaifa ni Umoja wa Tanzania, wimbo uliolenga kupatanisha mgogoro wa kisiasa kati ya vyama vya CCM na CUF. Mbali na wimbo huo, Nature ametoa nyimbo nyingi zenye mafunzo na ujumbe wa kizalendo kwa Taifa. [1][2]
Remove ads
Albamu alizotoa
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads