Trakoma

From Wikipedia, the free encyclopedia

Trakoma
Remove ads

Trakoma (inaitwa pia: vikope, Egyptian ophthalmia[1]) ni ugonjwa wa maambukizi unaosababishwa na bakteria Klamidia trakomati.[2] Maambukizi husababisha kukwaruza kwa sehemu ya ndani ya vigubiko vya macho. Huo mkwaruzo unaweza kusababisha maumivu ya macho, kuharibika kwa sehemu ya nje ya macho au konea, na hatimaye upofu.[2]

Thumb
Trakoma
Ukweli wa haraka Kundi Maalumu, ICD-10 ...
Remove ads

Kisababishi

Bakteria inayosababisha ugonjwa unaweza kusambazwa kwa mgusano wa macho au mapua wa moja kwa moja au usiokuwa wa moja kwa moja na mtu aliyeambukizwa.[2] Mgusano wa macho au mapua usiokuwa wa moja kwa moja unajumuisha kupitia nguo au inzi walioguza mtu aliyeambukizwa.[2] Maambukizi mengi huhitajika kwa zaidi ya miaka mingi kabla ya alama iliyoko kwa kigubiko cha jicho haijakuwa kubwa kwamba kope za macho zinaanza kukwaruza jicho.[2] Watoto husambaza ugonjwa kila mara zaidi ya watu wazima.[2] Mazingira chafu, maeneo yaliyo na watu wengi, na pasipo na maji safi ya kutosha na choo yanachangia usambazaji.[2]

Remove ads

Kinga na tiba

Juhudi za kuzuia ugonjwa unajumuisha uboreshaji wa kupata maji safi na kupunguza idadi ya watu walioambukizwa kupitia matibabu ya antibiotiki.[2] Hii inaweza kujumuisha kutibu, wote mara moja, vikundi vyote vya watu vinavyofahamika kuwa na ugonjwa huu kila mara.[3] Kufua nguo haitoshi kuzuia ugonjwa lakini inaweza kuwa bora na hatua zingine.[4] Aina za matibabu hujumuisha azithromycin ya kunywa au tetracycline ya tropikali.[3] Azithromycin hupendelewa kwa sababu inaweza kutumika kama dozi moja tu ya kunywa.[5] Baada ya mkwaruzo wa kigubiko cha jicho kutokea upasuaji unaweza kuhitajika ili kurekebisha sehemu ya kope za macho na kuzuia kuwa kipofu.[2]

Remove ads

Epidemiolojia

Ulimwenguni, takriban watu milioni 80 wako na maambukizi ya hivi karibuni.[6] Katika maeneo mengine maambukizi yanaweza kuwepo kwa ukubwa wa kati ya asilimia 60–90 ya watoto na mara nyingi huathiri wanawake kuliko wanaume kwa sababu ya kuwa karibu na watoto.[2] Ugonjwa huu ni ksababishi cha ukosefu wa kuona vizuri kwa watu milioni 2.2 ambapo milioni 1.2 ni vipofu kabisa.[2] Hutokea mara nyingi kwa nchi 53 za Afrika, Asia, Amerika Kusini na ya Kati na karibu watu milioni 230 wako hatarini.[2] Inachangia hasara ya dola bilioni 8 ya kiuchumi kila mwaka.[2] Ni ya kikundi cha magonjwa kinachojulikana kama magonjwa ya tropikali yasiyozingatiwa.[6]

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads